Huku ulimwengu ukijiandaa kuadhimisha Siku ya Furaha
Duniani ya Umoja wa Mataifa tarehe 20 Machi.
Tanzania ni miongoni mwa nchi
kumi za mwisho kwa viwango vya furaha kwa mujibu wa Ripoti ya Viwango vya
Furaha Duniani ya 2016 ambayo imetolewa mjini
Roma Italia.
Orodha hiyo iliandaliwa kwa kuangazia pato la mtu kwa
kila mwaka, miaka ambayo mtu anatarajiwa kuishi, kuwa na mtu wa kutegemea kwa
usaidizi, dhana ya kuwepo uhuru wa kufanya maamuzi maishaji, uhuru kutoka kwa
ufisadi, na ukarimu miongoni mwa mengine.
Mataifa yaliyo kwenye kundi la
mataifa kumi ya mwisho ni Madagascar, Tanzania, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin,
Afghanistan, Togo, Syria huku Burundi ikishika mkia.
Tanzania imo nambari 149 kati ya
nchi 157 ikiwa na alama 3.695 kati ya alama 10 na Rwanda nambari 152 na alama
3.315.
Uganda imo nambari 146 na alama
3.739, Malawi nambari 132 na alama 4.156, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imo
nambari 125 na alama 4.272 na Kenya nambari 122 na alama 4.356.
Somalia imo nambari 76 na alama
5.44.
Orodha hiyo imetayarishwa na
shirika la maendeleo endelevu ya Sustainable Development Solutions Network
(SDSN) ambalo lilianzishwa na Umoja wa Mataifa.
Denmark inaongoza kwa viwango vya
furaha duniani ikiwa na alama 7.526 ikifuatwa kwa karibu na Uswizi, Iceland na
Norway.
Finland, Canada, Uholanz, New
Zealand, Australia na Sweden zinafunga kumi bora.
Marekani imo nambari 13 na
Uingereza nambari 23.
0 comments:
Post a Comment