Tuesday, 8 March 2016

SAMAKI HATARINI KUTOWEKA AFRIKA..!

Mazao ya samaki yapo hatarini kutoweka barani Afrika, ikiwamo Tanzania iwapo mfumo wa usimamizi katika sekta ya uvuvi hautaboreshwa.

Mtaalamu wa masuala ya uvuvi endelevu Profesa Martin Tsamenyi, aliwaambia wanahabari na jopo la wataalamu wa sekta hiyo hivi karibuni kuwa, idadi ya samaki inazidi kupungua ulimwenguni kutokana na kukithiri kwa uvuvi haramu.
Profesa Tsamenyi kutoka Kituo cha Taifa cha Usalama wa Rasilimali za Bahari Australia, amesema asilimia nane ya samaki ulimwenguni huharibiwa, asilimia 52 hutumika na asilimia 19 kuvuliwa kupita kiwango kinachotakiwa.
Amesema uharibu huo ulitokana na mifumo mibovu ya usimamizi wa rasilimali hizo na uhuru wa kuvua kwenye kina kikuu cha bahari, mifumo ya kisheria na utawala wa sekta ya uvuvi, madhara ya utandawazi na Serikali kushindwa kusimamia uvuvi.
Profesa huyo amesema nchi hizo zimejikuta zikipoteza samaki wengi kila siku, baada ya meli kubwa kutoka mataifa yaliyoendelea ya Asia na Ulaya kuvua kwa wizi katika maeneo ya ndani ya mipaka inayoelezwa kisheria.

Profesa Tsamenyi amesema Serikali zinatakiwa kuzuia meli hizo haramu na njia hatari zinazotumika kuvua samaki na utunzaji wa mazingira.

0 comments:

Post a Comment