This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Tuesday 25 September 2012

Watanzania mabingwa wa kiswahili?

Kwa mpenzi yeyote wa Kiswahili ni sharti azingatie stadi nne za lugha hiyo. Yaani kuzungumza, kusoma kuandika na kuelewa lugha ya Kiswahili. Hata hivyo baadhi ya wakenya wamekuwa wakilamika kuwa vitabu vingi vya Watanazani vimekuwa vikitahiniwa nchini Kenya hususan katika vidato vya tatu na vinne. Ukweli ni kuwa Watanzania wamewabwaga wakenya na ipo mifano ya kutajika kuhusiana na hilo katika vitabu hususan vya fasihi. Swali ni je Wakenya wamepewa fursa ya kuandika au la? Ni nani anastahili kuwaambia waandike vitabu vya Kiswahili, na je wachapishaji vitabu wako radhi kuzichapisha kazi za Wakenya? Kuanzia miaka ya themanini hadi sasa, idadi ya vitabu vya Watanzania vilivyotahiniwa katika kunga za riwaya, tamthilia na ushairi ni kubwa kushinda vya Wakenya. Riwaya ya Kusadikika ya Shaaban Robbert(Mtanzania) ilitahiniwa mwanzoni mwa miaka ya tisini hadi mwaka 1994. Wakati huo hadi mwaka 1997 tamthilia ya Mashetani ya Ebarahim N. Hussein(Mtanzania) ilitahiniwa. Mwaka wa 1994 hadi mwaka 1998 riwaya ya Kisima cha Giningi ya Mohamed Said Abdullah(Mtanzania) ilitahiniwa. Katika miaka hiyo kuanzia mwaka 1998 tamthilia ya Amezidi ya Said Ahmed Mohamed (Mpemba) ikaanza kutahiniwa kuchukua mahali ya tamthilia ya Buriani ya A. S Yahya na David Mulwa(Wakenya). Wakati huo Mkenya Khaemba Ongeti alijipenyeza na tamthilia yake ya Visiki. Hayakuishia hapo, baada ya tamthilia za Visiki na Amezidi kuondolewa katika ratiba ya shule za upili nchii Kenya ikaingia riwaya nyigine ya Mohamed Said Ahmed (Mpemba) ya Kitumbua kimeingia mchanga. Na hiyo ilipoondoka ikaja riwaya ya Utengano ambayo inatahiniwa hadi sasa. Ukweli unaojitokeza hapa ni kuwa taasisi ya elimu nchini haiviteui vitabu hivyo kwa sababu ni vya Watanzania. Ni kutokana namna vilivyosukwa kimaudhui na kifani.Isitoshe waandishi wa vitabu hivyo wameandika wameandika vitabu vingi tu. Kwa mfano Said Ahmed Mohemed ameandika zaidi ya vitabu 40 vya Kiswahili. Mohamed Said Abdullah ameandika vitabu vingi tu kama vile Kisima cha Giningi, Duniani kuna watu, Mizimu ya watu wa kale na Kadhalika. Hata hivyo ni vyema kutambua kuwa baadhi ya Wakenya wamejitokeza na kuandika kazi nzuri za fasihi ya Kiswahili kama vile Siku Njema ya Ken Walibora, Mstahiki Meya ya Timothy Arege na Kifo Kisimani ya Kithaka Wamberia. Kwa ufupi wapenzi wa Kiswahili katika kanda ya Afrika Mashariki wakijumuisha mataifa ya Rwanda, Sudan Kusini, Sudan, Somalia na Uganda waandike vitabu zaidi vya Kiswahili. Twasubiri siku watanzania watavitahini vitabu vya Kiswahili vya wakenya, Vivyo hivyo si dhambi kitabu cha Kiswahili kilichoandikwa na Mrundi ama Mnyarwanda kikitahiniwa Uganda na vinginevyo. Ni maoni tu!!!!

USOMAJI WA VITABU WAPUNGUA KWA SABABU YA MITANDAO YA KIJAMII???

Nimejikuta natafakari jambo hili na kuingia kwenye marumbano makubwa na serikali ya kichwa changu hasa nikiangalia hali halisi tunayoishi sasa. Mapinduzi ya kompyuta yamebadilisha sana maisha. Enzi zile hata ukipewa assignment darasani unakimbia maktaba kutafuta kitabu. Siku hizi mambo yamebadilika. Hata assignment inapotolewa wanafunzi wanakimbilia kwenye Internet maana vitu vinapatikana kwa urahisi zaidi. Najiuliza kwa staili hii kweli watu hasa walio na access ya Internet wastani wao wa kusoma vitabu ukoje? Ripoti moja ilishawahi kuonyesha kuwa ujio wa smartphone na mitandao ya kijamii inawashawishi sana watoto wasome vitabu. Ilinipa wakati mgumu sana kuitafakari ripoti hii iliyotolewa kutokana na utafiti mmoja nchini Marekani. Nikiangalia mazingira yetu inanipa wakati mgumu sana kuamini jambo hilo. Naona kama vile uwezo na hamu ya watu kusoma vitabu unapungua zaidi wakipendelea kuingia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kusoma hiki na kile! Hii ndiyo Teknolojia Yetu…

Sunday 23 September 2012

HUTOKA KIWALENIIii HIKI HAPA KICHWA KINGINE...(KIWA WA 2)ANAWAKILISHA DH CREW-MWITE HUBE KIWA...

SIKILIZA NGOMA YAO HAPAA INAITWA SIKUDHANI...
HUBE KIWA(sapremo wa kili)ANAWAKILISHA DH.CREW(ODEO & HUBE)

Tuesday 18 September 2012

TAHADHARI KWA WATUMIAJI SIMU ZA MKONONI

Simu zinatumia Mionzi ya MICROWAVE ambayo huwezesha kuunganisha simu yako kwenda kwenye Mnara na mnara huunganisha Simu yako na Mitambo ya Mtandao wako ambapo pia Hurudishwa kwenye mnara hadi kwa mtu Unaye mpigia. Microwave ndio njia kuu ya muunganisho huo Lakini kunamdhara mengi mtu huyapata kutokana na kuwa karibu na Mionzi hiyo ambayo hadi sasa bado haijafahamika ni kwa kiasi Gani. Uchunguzi umeonyesha kuwa kuna madhara mengi ya kiafya tunayapata kutokana na Matumizi ya simu. mfano wa magonjwa hayo ni 1.KUUMWA KICHWA MARA KWA MARA 2PRESSURE YA KUPANDA NA KUSHUKA 3.UVIMBE KWENYE UBONGO 4.KANSA 5.ALZHEIMER 6.NA MENGINE MENGI Hatuwezi kujizuia kutumia simu na Hatuwezi kuzuia hiyo mionzi ya MICROWAVE sababu ni sehemu ya shughuri zetu za kila siku ila tunaweza KUPUNGUZA. hapa nawaletea Njia chache za kupunguza Mionzi ya MICROWAVE isituletee matatizo makubwa zaidi. 1.Punguza matumizi yasio lazima ya simu. Mfano Ongea mda mfupi kwa kutumia simu sio muda mrefu uweunaongea,Uchunguzi umeonyesha kuwa ukiongea kwa DAKIKA mbili haileti madhara, (Alter natural electricity of the Brain) 2.Watoto wasiruhusiwe kutumia Simu bali pale tu inapobidi. 3.Tumia Earphone za wireless mfano za bluetooth. ni nzuri zaid kuliko za wire,Earphones za wire zinaongeza wingi wa mionzi sababu pia zinatumika kama antena ya simu, 4.Usiweke simu kwenye Mfuko wa suruari au shati au kiunoni,sehemu za mwili zinapitisha mionzi vizuri zaidi sababu pia ni njia ya neva za ubongo na chini ya mwili. 5.Usitumie simu kwenye chumba kidogo au lift au gari. Sababu Simu itatumia nguvu nyingi kuvuta mionzi ili kuwezesha mawasiliano. 6.Ukipiga simu subiri hadi mtu apokee ndipo uweke sikioni kusikiliza na sio wakati ina connect. 7.Usipige simu kama network ipo chini au signal inaonyesha bar moja au ndogo, simu itavuta mionzi zaidi ili kufanya mawasiliano 8.Ukinunua simu hakikisha unasoma kama ina LOW SAR (Specific Absorbtion Rate) Ni kipimo cha kupokea mionzi ya simu Za nokia zinazo ila za Kichina HAZINA. 9.Tumia vifaa vya kupunguza Mionzi vinapatikana madukani (vinawakawaka taa hivi) 10.Weka simu atleast 3.4 inches kutoka kwenye sikio 11.Jitahidi kutumia Earphones muda wote unapotumia simu 12.Tumia speaker phone."Loudspeaker " 13.Text zaidi kuliko kupiga simu . 14.Jitahidi usitumie muda mwingi kwenye simu kama umeiweka kwenye sikio 15.Jitahid kuiweka mbali na reproduction organs zako hasa kwa wanaume ambao hatujapata watoto.

SIMU ZA MKONONI NA KANSA YA UBONGO: BALAA JINGINE KWA AFRIKA?

Kwa muda mrefu kumekuwa na mjadala mkali kuhusu nguvu za mionzi ya mnunurisho inayotolewa na simu za mkononi kama zinaweza kusababisha kansa ya ubongo ama la. Hatimaye Shirika la Afya Duniani limetoa tamko kuhusu utafiti unaoonyesha kwamba simu za mkononi zinaweza kuwa zinasababisha kansa ya ubongo. Hatari hii inasemekana kuwa ni kubwa zaidi kwa watoto wadogo na matineja kwani mafuvu yao bado hayajakomaa sawasawa. Naomba hii isiwe kweli kwani kama tunavyojua, Afrika ndiyo jalala la bidhaa feki, mbovu na zilizoisha muda wake. Bila shaka nitakuwa sahihi nikisema kwamba simu zinazotoa mionzi hatarishi kwa binadamu na zitakazokuwa zimepigwa marufuku sehemu zingine za dunia ndizo zitarundikana Afrika. Kama utafiti huu ni wa kweli basi miongo kadhaa tu ijayo Afrika itakumbwa na mripuko wa kansa ya ubongo – mojawapo ya kansa hatari kabisa na inayohitaji tiba ghali sana! Tunachoweza kufanya kwa sasa ni kufuata mapendekezo yaliyotolewa yakiwemo kununua simu zisizotoa mionzi mikali zaidi, kuweka simu mbali na sikio wakati wa maongezi na kwa wenye uwezo kununua vifaa vinavyosafirisha mawimbi ya sauti kama “Bluetooth”. Vifaa hivi huwekwa sikioni na vinaweza kudaka mawimbi ya sauti ya simu iliyowekwa mfukoni au sehemu nyingine na kuyasafirisha sikioni kwa msikilizaji bila madhara yo yote.

Monday 17 September 2012

Elinaja kijana aliyeamua kuandika bongo fleva kwenye mtihania atoa single yake mpya akimshirikisha barnaba.


Bado Tanzania haijamsahau huyu mwanafunzi ambae aliongelewa sana wakati matokeo ya form IV yalipotoka mwaka jana kutokana na kuandika mistari ya bongofleva kwenye mtihani wake baada ya kuona hakuna chochote alichopata kwenye elimu.
Elinaja alisema  aliamua kuandika mistari ya bongofleva ili wahusika wapate msg, hata hivyo alisema kitu ambacho ana uhakika uwezo wa kukifanya anao ni muziki ambapo amerekodi upya single yake ya Mr President na kumshirikisha Barnaba, bonyeza play hapo chini kumsikiliza na kudownload.

Monday 10 September 2012

Faida za Tende Mwilini Mwako.

Je unajua kwamba tende ndio tunda pekee lenye kuupatia mwili vitu vinne kwa wakati mmoja, vitamin,protini,wanga na mafuta?. Mbali na utamu wake tende ambazo hulika sana Mwezi wa Ramadhan zina faida nyingi sana kwa mwili wa binadamu. Ebu zijue faida zake……. Tende ni tunda ambalo linayeyuka kirahisi tumboni, na lenye faida nyingi sana ambazo hulifanya liwe tunda la kipekee. Baadhi ya faida zake mwilini ni kama ifuatavyo: 1-Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye tende,husaidia kurekebisha matatizo ya tumbo na huleta ahueni kwa watu wenye matatizo ya kupata choo. 2-Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu,ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki,moyo wako utakuwa imara. 3-Tende husaidia pia kwenye mambo ya malavi davi. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali,kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina za kufanya mapenzi. 4-Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba,wakati mwanamke anapokaribia kujifungua,hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa kujifungua. 5-Wataalamu wa vyakula, wanazichukulia tende kama chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha,kwani husaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu vinavyomfanya mtoto awe na afya njema. 6-Tende husaidia kupunguza kiwango cha kilevi (alcohol) kwenye damu. Maji ya kunywa ambayo tende imelowekwa ndani yake husaidia kuondoa haraka alcohol mwilini. 7-Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee,na pia husaidia kurekebisha ngozi na huondoa mabaka ya kuungua na jua. 8-Kutokana na madini ya chuma kwenye tende,watu wenye upungufu wa damu hupata ahueni. 9-Vitamin B1 na B2 zilizopo kwenye tende,husaidia kuyapa nguvu maini. 10-Tende pia huleta ahueni kwa watu wenye kikohozi na mafua.