Habari
ya mzaha kwamba wanaume wa taifa la Eritrea wameagizwa kuoa wake wawili, ambayo
imesambaa barani Afrika imewaudhi maafisa wa taifa hilo.
Afisa mmoja wa ubalozi wa Eritrea
Kenya ameiambia BBC kuwa,hata mwendawazimu katika mji mkuu wa Asmara atajua
kwamba habari hii sio ya kweli.
Habari hiyo ilichapishwa katika mtandao wa kitengo cha
gazeti la The Standard la Kenya cha Crazy Monday.
Baadhi ya watu wametoa maoni yao katika mtandao wa
Twitter kwamba wako tayari kusafiri hadi Eritrea ili kutafuta wanawake wa kuoa.
Jarida la Crazy Monday ambalo
huchapishwa na gazeti la Standard, hujulikana sana kwa stori zake za udaku,
likiwa ni mpango wa kutaka kuwavutia vijana.
Lakini hilo halijazuia taarifa hiyo kuripotiwa katika
mataifa ya Nigeria hadi Afrika Kusini huku wengine wakisema kuwa ni ukweli.
Habari hiyo inasema kwamba ili
kuhakikisha kuwa kuna wanaume walio wachache nchini humo wanaokidhi mahitaji ya
wanawake walio wengi, kufuatia vita kati ya taifa hilo na Ethiopia mwaka
1998-2000, kila mwanamume lazima aowe wake wawili la sivyo afungwe jela.
Lakini afisa wa ubalozi wa
Eritrea aliyezungumza na BBC amesema idadi ya wanawake na wanaume inakaribiana.
Waziri wa habari nchini Eritrea
Yemane Gebremeskel, alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter akisema kwamba
habari hiyo ni ya uvumi sio ya kweli na inakera.
0 comments:
Post a Comment