Rais
wa Ufaransa Francois Hollande amemsamehe mwanamke aliyekuwa amefungwa jela
miaka 10, kwa makosa ya kumuua mumewe kwa kumpiga risasi tatu.
Mume wa Jacqueline Sauvage
alikuwa mlevi aliyezoea kumpiga, na alikuwa amembaka yeye na mabinti zake kwa
miaka mingi.
Jacqueline amesema mumewe huyo
pia alimnyanyasa mtoto wao wa kiume, ambaye baadaye alijiua.
Watu zaidi ya laki 4 walikuwa
wametia saini ombi la kumtaka Bw Hollande, amwachilie huru mwana mama huyo.
Mawakili wa Mwanamke huyo mwenye
umri wa miaka 68, wamesema anatazamiwa kuondoka gerezaji katikati mwa mwezi
Aprili.
Siku ya tarehe 10 Septemba 2010 siku
ambayo mwanawe alijiua kutokana na manyanyaso ya baba yake, mwana mama huyo alimpiga
risasi mumewe mara tatu akitumia bunduki.
Alipatikana na hatia na kufungwa
jela miaka 10 gerezani Oktoba 2014, na kifungo chake kikatizamwa upya Desemba
2015, baada ya rufaa yake ya kujitetea akisema kwamba alikuwa anajikinga
kukataliwa.
Kesi hiyo ilifuatailiwa sana nchini
humo,wengi wakitaka haki ya kutumia sababu ya kujikinga kujitetea iwekwe wazi
zaidi.
Walitaka watu walionyanyaswa na
kudhulumiwa nyumbani, waruhusiwe kutumia haki hiyo kujitetea.
Bw Hollande amefanya uamuzi wake
siku mbili, baada ya kukutana na mabinti watatu wa mwana mama huyo.
0 comments:
Post a Comment