Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala inalazimika kununua maji ya
chupa,
kwa ajili ya kusafisha vifaa vya upasuaji baada ya mashine mbili za
kuchujia maji kuharibika.
Hayo yamesema jana na katibu wa afya
wa hospitali hiyo Willborada Athanas,wakati akipokea mashine moja ya kuchujia
maji iliyotolewa na kampuni ya Tanzania Water Equipment Supply Company (
Twesco).
Amesema kwa kipindi cha miezi mitatu
sasa hospitali hiyo inalazimika kununua maji kwa ajili ya kusafishia vifaa vya
upasuaji, licha ya mashine moja kuuzwa Sh5.6 milioni.
Ameongeza kuwa kila baada ya wiki mbili wanalazimika kununua lita
60 za majisafi ambazo ni sawa na Sh 52,000, kwa ajili ya kusafishia vifaa.
Amesema mashine ya kwanza iliharibika
miezi sita iliyopita na mtaalamu alipopelekwa kwa ajili ya kutengeneza,
aligundua kuwa imeharibika na haifai kutengenezwa huku mashine ya pili
ikiharibika miezi mitatu iliyopita na hivyo kusababisha changamoto kubwa katika
kitengo cha upasuaji.
Amesema licha ya hospitali hiyo
kupandishwa hadhi na kuwa ya rufaa, bado mfumo wa majitaka haukidhi mahitaji.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Twesco Victor
Manyanga amesema kuwa, mashine waliyokabidhi ina uwezo wa kusafisha lita 300 za
maji kwa siku.
0 comments:
Post a Comment