Raia wa Nchi za Afrika
Mashariki wataanza kutumia paspoti za kielektroniki ambazo zitatumika
kurahisisha usafiri kwa wananchi wa eneo hilo.
Hayo yamedokezwa na Mkuu
wa awasiliano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Owora Richard Othieno ambaye
ameongeza kuwa, kuanzia mwezi Machi, raia wa nchi za Afrika Mashariki wanaweza
kupata pasi za kusafiria za kielektroniki za jumuiya hiyo ya kiuchumi, ili
kusahilisha usafiri katika nchi hizo.
Owora Othieno amedokeza
hayo kabla ya mkutano wa 17 wa viongozi wa nchi za EAC unaopangwa kufanyika
tarehe 29 mwezi huu huko Arusha, Tanzania. Amesema, viongozi wa kanda hiyo
watazindua pasi hiyo, ambayo itakuwa moja ya hatua muhimu katika kufikia lengo
la kuimarisha ushirikiano wa kikanda.
Wananchi wa Afrika
Mashariki wamekuwa wakisubiri pasi hiyo kwa muda mrefu na hivyo kuzinduliwa
kwake ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa nchi tano wanachama
ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.
Katika kikao cha mwezi
huu, wakuu wa EAC watajadili ombi la Somalia kutaka kujiunga na jumuiya hiyo.
0 comments:
Post a Comment