Halmashauri ya
Tunduma Mkoa wa Songwe, imeyafungia maduka
manne yanayotuhumiwa kuuza kadi za
kliniki zenye maneno yaliyoandikwa ‘haziuzwi’.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Halima Mpita, amesema kuwa wameyafunga
maduka hayo baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi, juu ya
watumishi wa Kituo cha Afya cha Tunduma kuwaamuru wanunue kadi hizo kinyume na
sheria kwa watu binafsi, wakati zinapaswa kutolewa bure kwenye vituo vya afya,
zahanati na hospitali.
Mpita amesema baada ya kupata malalamiko hayo, alituma timu ya wakaguzi
kwenda kwenye maduka hayo yaliyo jirani na kituo hicho kubaini kufanyika kwa
biashara hiyo haramu.
Mkurugenzi huyo ameutaka
uongozi wa halmashauri hiyo, kuendelea kufuatilia huduma za afya katika
zahanati zinazozunguka mji huo.
Awali wananchi
walilalamika kuuziwa kadi moja kwa Shilingi elfu 2, wakati zinapaswa kutolewa
bure kwa wajawazito.
Mkazi wa Mtaa wa Sogea Farida Sichone, amesema kwa muda mrefu wamekuwa
wakilazimishwa kununua kadi hizo.
0 comments:
Post a Comment