Raia wa Switzerland Gianni Infantino
amechukua mahala pake Sepp Blatter kama rais wa shirikisho la soka duniani
Fifa.
katibu huyo mkuu wa Fifa alipata
kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wake wa
karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.
Mwanamfalme Ali bin al-Hussein
alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa kupata hata
kura moja.
Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya
kura kuanza kupigwa mjini Zurich.
Raundi ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kum'baini
mshindi wa moja kwa moja.
Wingi wowote wa kura[zaidi ya
aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa unaweza kumwezesha
mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.
Infantino ni wakili mwenye umri
wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland ,ikiwa ni
eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter.
Blatter ambaye aliliongoza
shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya kupigwa
marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha miaka sita .
Baada ya kutangazwa
mshindi, Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea
kutokana na hisia alizokuwa nazo.
Lakini aliwaambia
wajumbe kwamba ''kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya
Fifa''.
0 comments:
Post a Comment