Madeni yanayoizunguka
serikali ya Marekani yanakaribia dola
trilioni 20, na kuna hofu ya kuongezeka
zaidi madeni hayo.
Kwa mujibu wa takwimu
rasmi ni kwamba Washington inadaiwa dola trilioni 19.8, kiasi ambacho ni sawa
na asilimia 103 ya pato jumla la taifa.
Inatazamiwa kuwa kufikia
mwaka 2017 wakati kama huu, madeni ya Marekani yatapanda na kufikia dola
trilioni 20.
Kufuatia takwimu hizo
Marekani kwa sasa inahesabiwa kuwa nchi yenye madeni mengi zaidi duniani.
Suala hilo ni kinyume
kabisa na mtazamo wa watu wengi ambao hudhani kuwa Marekani ni nchi tajiri na
isiyoweza kukopa.
Serikali ya Washington
imekopa dola trilioni 13.7 kutoka kwa mashirika na watu binafsi na vilevile
ikakopa dola trilioni 5.3 kutoka kwa hazina ya taifa.
Duru zinaarifu kuwa
tangu kuanza kupindi cha uongozi wa Rais Barack Obama, madeni ya Marekani
yameongezeka maradufu.
0 comments:
Post a Comment