Friday, 12 February 2016

INDIA YAZINDUA BUNDUKI NYEPESI DUNIANI….

Miaka miwili baada ya India kuzindua Nirb heek bunduki inayodaiwa kuwa ya kwanza ya
wanawake, kiwanda cha kutengeza silaha cha taifa hilo kimezindua bunduki kama hiyo na kusema ndio bunduki nyepesi zaidi duniani.
Bunduki hiyo ina gramu 250 na inauzwa dola 513,tofauti na Nirb heek iliyouzwa kwa bei ya juu ya dola elfu 1 na 990.
Watengezaji wake wanasema kuwa Nidar imeundwa kwa kutumia alumini, ambayo inaifanya kuwa nyepesi zaidi lakini bado ina nguvu sawa na ile ya chuma.
Urefu wake ni wa milimita 140 ambao unaifanya kuweza kutosha katika kiganja cha mkono.
Bunduki zote mbili Nirb heek na Nidar, zina maana ya Nirbhiya jina la utani alilopewa Jyoti Sign na vyombo vya habari, ikiwa ni mwathiriwa wa genge la ubakaji katika basi moja mjini Delhi mwaka 2012.
Majina yote matatu yanamaanisha jasiri kwa lugha ya Kihindi.

Hutengezwa na viwanda vya serikali, na watengezaji wake wanasema kuwa zitawasaidia watu kutokuwa na uwoga na jasiri.

0 comments:

Post a Comment