Friday 19 February 2016

SIMBA WATOROKA MBUGA NA KUINGIA MTAANI..!!

Simba wasiojulikana idadi yao, wametoroka mbuga ya taifa ya wanyamapori ya Nairobi.

Tayari shirika la wanyama pori la Kenya KWS, limeanzisha oparesheni ya kuwasaka wanyama hao.
Shirika hilo limewataka wakaazi wa maeneo hayo kutahadhari, huku taarifa zinasema mara ya mwisho walionekana eneo la makazi la Langata.
Hii si mara ya kwanza kwa wanyama hao kuzua taharuki katika eneo hilo.
Langata ni eneo lililo na watu wengi, na maafisa wa KWS pamoja na polisi wanahofia kwamba wanyama hao huenda wakasababisha hasara, iwapo hawatapatikana haraka na kurudishwa katika mbuga hiyo.

Simba sita waliripotiwa kutoroka katika mbuga hiyo Alhamisi jioni, lakini wanne kati yao walipatikana 

0 comments:

Post a Comment