Tuesday, 2 February 2016

TAI KUTEKA NDEGE ZISIZOKUWA NA RUBANI UHOLANZI..!!

Maafisa wa polisi nchini Uholanzi, wameanza kuwafunza tai kuteka ndege zisizokuwa na rubani zikiwa angani.

Katika video moja iliyochapishwa kwenye mtandao, Tai anaonekana akiitwaa ndege moja isiyokuwa na rubani kwa makucha yake angani na kupaa nayo.
Hii ni baadhi tu ya mbinu zinazojaribiwa na maafisa wa polisi nchini Uholanzi, kukabiliana na kuenea kwa matumizi ya ndege zisizokuwa na rubani zinazorushwa angani bila idhini.
Polisi walishirikiana na kampuni moja ya Guard From Above kuwafunza tai hao.
Tai hao wanafunzwa kuteka nyara ndege hizo ziosizokuwa na rubani kwa kudhania kuwa ni mlo.
Tai hao wanafunzwa kuchukulia ndege hizo zisizokuwa na rubani kama mlo hivi, na hivyo kama kawaida wanaiteka kwa haraka na kuificha mbali taarifa hiyo ya polisi inasema.
Ndege hizo zisizokuwa na rubani zimekuwa nyingi sana angani Uholanzi, na sasa maafisa wanaosimamia usalama wa ndege nchini humo, wanasema zinatishia usalama wa ndege zinazowabeba abiria.
Majuzi tu nusura ndege moja isiyokuwa na rubani isababishe ajali mbaya.

Vilevile kuna hofu kuwa ndege hizo huenda zikatumiwa na magaidi, kutekeleza mashambulizi ama hata kupeleleza majengo lengwa.

Related Posts:

  • MVUA YALETA MAAFA WILAYANI MPWAPWA… Watu wanne wakiwamo watatu wa familia moja ambao ni wakazi wa Kijiji cha Isighu kitongoji cha Majumba Sita wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wamekufa maji baada ya makazi yao kusombwa na mvua iliyo nyesha usiku wa kuamkia Ja… Read More
  • MWENYEKITI WA CCM MBEYA ANUSURIKA KUUAWA.. Mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini, Efrahim Mwaitenda mwenye umri wa miaka 60 amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mgongoni na mtu au watu wasiofahamika. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula amesema tukio hilo li… Read More
  • SERIKALI: UZALISHAJI WA CHAKULA UTAFIKIA TANI MILIONI 3 Serikali imefanya tathmini ya awali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini na kubaini kuwa uzalishaji wa chakula nchini utakuwa na ziada ya tani 3,013,515. Hayo yamesemwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles … Read More
  • AHUKUMIWA KIFUNGO KWA KULALA NA MPENZI WA MWANAE… Mwanamke mmoja ambaye ametambulika kwa jina la Alaine Goodman (46) amehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kufanya mapenzi na kijana mwenye umri mdogo ambaye ni mpenzi wa mtoto wake. G… Read More
  • SUDAN YAPINGA AMRI YA TRUMP..! Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Sudan imemuita mwanabalozi wa Marekani mjini Khartoum kupinga hatua ya Rais Donald Trump ya kuwapiga marufuku raia wa nchi hiyo kuingia Marekani. Sudan inasema kuwa hatua hiyo… Read More

0 comments:

Post a Comment