Tuesday, 16 February 2016

VIRUSI VYA ZIKA VYAPATIKANA KATIKA UBONGO…!!

Ushahidi zaidi unaohusisha virusi vya Zika na kasoro ya maumbile miongoni mwa watoto
umepatikana, wanasayansi nchini Brazil Wamesema.
Wasayansi hao kutoka chuo kikuu cha PUC-Parana University wamegundua virusi hivyo ndani ya ubongo wa watoto wawili ambao waliishi kwa saa 48 pekee.
Virusi hivyo vinavyosababishwa na mbu vinasababisha kasoro ya watoto kuwa na vichwa vidogo mbali na ubongo ulioharibika.
Brazil ina takriban visa 460 vya ugonjwa huo na inachunguza visa vingine 3,850.Virusi hivyo vimesambaa katika eneo la Marekani kusini,lakini Brazil imeathiriwa zaidi.
Wanasayansi wameeleza kwamba violezi vilivyochukuliwa kutoka kwa ubongo wa watoto hao, vilionyesha kuwa virusi hivyo vya Zika vilikuwa hai ndani ya ubongo.
Wanasayansi hao wamekuwa wakifuatilia mimba za wanawake 10 wajawazito katika jimbo la Kaskazini mashariki mwa Paraiba, ambalo ni la pili kwa visa vya ugonjwa huo.

Related Posts:

  • TANZANIA KINARA WA SOKO LA SIMU AFRIKA… Ripoti ya mwaka 2016 ya Uchumi wa Simu za Mikononi Afrika inasema kuwa, Tanzania ni miongoni mwa nchi nane Afrika zenye soko kubwa la simu za mikononi. Ripoti hiyo iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana kwenye mk… Read More
  • UTAFITI:UNENE UNAUA MAPEMA…!!   Utafiti wa kimataifa umegundua kuwa kunenepa kunahusiana moja kwa moja na visa vya watu kufa mapema, huku wanaume wakiwa katika uwezekano mara tatu wa kufariki zaidi ya wanawake. Kwa kutumia data kutoka takriban … Read More
  • 2016 WAELEKEA KUWA MWAKA WENYE JOTO KALI KUWAHI KUREKODIWA..! Mwaka huu wa 2016 huenda ukawa ndio wenye joto kali zaidi kuwahi kurekodiwa, kufuatia hali ya joto duniani kuweka rekodi mpya ya viwango vya nyuzi joto katika miezi sita ya kwanza. Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Hali y… Read More
  • UNYONYAJI KIDOLE UNAFAIDA KWA WATOTO- UTAFITI Ripoti mpya inasema watoto wanaonyonya vidole au kung'ata kucha zao kwa meno huenda wasipate matatizo ya kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani. Kwa mujibu wa waandishi katika jarida la Pedi… Read More
  • PANYA SASA KUTUMIA UZAZI WA MPANGO…! Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), kimepata suluhisho la kupunguza kuzaliana panya nchini kwa kuanzisha uzazi wa mpango kwa wanyama hao. Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam Mtaalamu wa Kilimo w… Read More

0 comments:

Post a Comment