Takriban
wanandoa 3000 kutoka kote duniani wameshiriki katika harusi ya halaiki katika
makao
makuu ya kanisa tata la kuwaunganisha watu Kusini mwa Korea.
Wengi wa wanandoa hao walikutana
siku chache tu kabla ya kufungishwa ndoa na mamlaka ya kanisa hilo kabla ya
sherehe hiyo ya jumamosi katika eneo la Gapyeong, kaskazini mashariki mwa
Seoul.
Harusi hiyo ambayo hufanyika kila
mara ilianza kufanyika miaka ya sitini.
Kanisa hilo lililoanzishwa na
marehemu Sun Myung Moon,limeshtumiwa kwa kuwadanganya waumini wake, swala
inalokana.
Sung Myung Moon alifariki mnamo
mwezi Septemba mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 92.
Anaheshimwa na wafuasi wake
wanaojiita Moonies.Wakosoaji wake wamemuelezea kuwa mtu muongo.
0 comments:
Post a Comment