Thursday 4 February 2016

HABARI TANO ZA TEKNOLOJIA AMBAZO HAZIFAI KUKUPITA..!

Teknolojia hubadilika mara kwa mara na kila siku kuna mambo mapya yanayovumbuliwa na mitindo pia kubadilika,hapa nimekuwekea habari tano kuhusu teknolojia ambazo hazifai kukupita.

1.Li-fi ina kasi mara 100 zaidi ya Wi-fi
Teknolojia mpya ya kutuma data ijulikanayo kama Li-fi imefanyiwa majaribio.
Li-fi ina uwezo wa kumfanya mtumiaji kupata huduma ya mtandao mara 100 zaidi ya Wi-Fi na hutoa kasi ya hadi Gigabait moja kwa kila sekunde.
Li-Fi inahitaji mwangaza kama vile wa glopu,huduma ya mtandao na sensa ya picha
Ilijaribiwa wiki hii na Velmenni mjini Tallinn Estonia.
Velminni ilitumia glopu ya li-fi inayoweza kusafirisha data kwa kasi ya Gigabait moja kwa sekunde.
Jaribio la maabara limeonyesha kuwa li-fi ina kasi ya hadi Gigabait 224 kwa sekunde.
Ilijaribiwa katika afisi ili kuwasaidia wafanyikazi kupata huduma ya mtandao na katika kiwanda ambapo iliweka mwangaza.
2.Choo kinachojifungua na kujiosha
Choo cha kisasa ambacho kina uwezo wa kujifungua unapokaribia na pia kujiosha, ni moja ya vitu vinavyoonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya teknolojia mpya za bidhaa za elektroniki Las Vegas.
Choo hicho kilichopewa jina Neorest, pia humsafisha anayekitumia kwa kifaa kinachotoa maji moto na hewa mtu akiwa ameketi.
Pia kina teknolojia inayokiwezesha kuua bakteria na virusi.
Licha ya choo hicho kuuzwa $9,800 (£6,704), waliotengeneza choo hicho vyoo zaidi ya 40 milioni vya miundo ya awali vimeuzwa.
Kampuni ya Toto iliyotengeneza choo hicho, imesema muundo huo wa sasa bado unaendelea kuboreshwa.
"Huhitaji kuosha bakuli la choo kwa kipindi cha mwaka mmoja,” anasema msemaji wa Toto, Bi Lenora Campos.
Choo hicho hata hivyo si kwamba kitakuondolea kabisa majukumu yote ya usafi chooni,kwani hakiwezi kujiosha upande wa nje iwapo kutakuwa na uchafu.
Maonyesho hayo ambayo kwa Kiingereza yanajulikana kama Consumer Electronics Show hufanyika kila mwaka ambapo kampuni mbalimbali na wavumbuzi huonyesha teknolojia za karibuni zaidi.
3.Mercedes yazindua lori linalojiendesha
Amini usiamini huku watu wengi Afrika Mashariki wakilazimika kulipa mabilioni ya shilingi ilikujifunza kuendesha magari, teknolojia sasa imepiga hatua moja zaidi.
Mwanzo ilikuwa ni magari madogo sasa kampuni ya kutengeneza magari ya kifahari Daimler Mercedes-Benz imezindua lori linalojiendesha lenyewe!

Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo yenye asili yake nchini Ujerumani Wolfgang Bernhard alibofya kidude na mara lori likachukua usukani na kuenda lenyewe pasi na kusababisha ajali ya aina yeyote.
Lori hilo linatumia teknolojia ya kamera kwa pamoja na 'radar' kukwepa magari mengine barabarani.
Aidha mtambo huo unatuma na kupokea taarifa na mawasiliano iwapo lori hilo linasogea karibu zaidi kitu chochote iwe ni gari, mti ama hata mtu barabarani.
Hata hivyo kampuni hiyo ilisisitiza kuwa sharti dereva awe hapo wakati wote kifaa hicho cha "highway pilot" kinapotumika kama tahadhari kusitokee ajali.
Lorry hilo aina ya Actross lilijaribiwa katika barabara inayotumika na uma ya Baden-Wurttemberg Ujerumani.
Kwa mujibu wa bwana Bernhard lori hilo lilimudu kujiendesha na hata kutimia kasi ya Kilomita 80 kwa saa.

Mkurugenzi huyo alikuwa na Waziri Winfried Kretschmann walikuwemo ndani ya lori hilo wakati wa jaribio hilo la kihistoria.

Bernhard alissistiza kuwa wakati dereva anapohisi amechoka gari hilo linaweza kuchukua usukani naye ajipumzishe kidogo japo kwa kutengeneza kikombe cha chai huku kamera na mfumo huo wa radar zikidhibiti usukani.
Mfumo huo unatumia miale kubaini kona na maelezo kwenye mabango barabarani.
''Kwa hakika hata uwe mstadi kivipi , mfumo huu wa "highway pilot" unaendesha vyema zaidi kuliko mwanadamu na hata iwe kwa kiwango kipi haiwezi kuchoka sawa na vile madereva wa malori huwa wanawachoka na kupoteza umakinifu barabarani.'' alisema mkurugenzi wa kampuni hiyo Wolfgang Bernhard.
4.Je una simu ya Android? Soma utafiti huu
Simu za kisasa zinazotumia mfumo wa Android zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi sana.
Uchunguzi umebaini kuwa simu zinazotumia mfumo huo zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi mno pasi na kutumia kifaa cha GPS yake.
Aidha simu hizo zinaweza kudukuliwa kwa kutumia matumizi ya betri yake huku utafiti ukisema kuwa simu zinazotumika karibu na kifaa cha kupeperushia masafa ya simu za kuungia mbali.
Simu za kisasa ''Smartphone'' hutumia nguvu zaidi inapokuwa mbali zaidi na kifaa hicho cha kupeperushia masafa ya GSM, kwani inachangamoto tele za kungamua masafa.
Matumizi ya nguvu zaidi ya shughuli zingine yanaweza kubaiishwa na ''alogarithm'' muundo msingi wa simu yenyewe.
Watafiti hao sasa wameunda mfumo ambao unakusanya habari kuhusu matumizi ya betri ya simu.
‘’Mfumo huo hairuhusu kutumia GPS wala huduma zozote kwa mfano mtandao wa Wi-fi ‘’
Jopo hilo linajumuishwa Yan Michalevsky, Dan Boneh na Aaron Schulman kutoka idara ya sayansi ya tarakilishi katika chuo kikuu cha Standford pamoja na Gabi Nakibly kutoka kwa kampuni ya Rafael waliandika katika utafiti wao.
‘’Tunaruhusa ya kuunganisha mtandao na upatikanaji wa nguvu yao.’’
‘’Hizi ni ruhusa za kawaida kwa mfumo huo na inawezekano wa kutoleta hutuma kwa upande wa mwathiriwa.
Kuna mifumo 179 ambazo zinapatikana kwenye Anaroid ,timu hiyo iliongezea.
Shughuli kama kuskiza muziki au kutumia mtandao wa kijamii inamaliza betri ya simu lakin i hii inaweza kupunguzwa kutokana na ‘’kujifunza kwa mashine’’ripoti inasema.
Jaribio hilo lilifanyiwa kwa simu ambazo zinatumia mtandao wa 3G lakini haikuweza kupima nguvu kwa kuwa twakimu inalindwa na kifaa hicho.
5.Samsung yakiri TV zake zinanasa sauti
Samsung imewaonya wateja wake kuhusu kutojadili mambo yao ya kibinafsi mbele ya televisheni zao.
Onyo hilo ni kwa wale watazamaji ambao hudhibiti televisheni zao kwa kutumia sauti.
Baadhi ya runinga hizo za kisasa husikiliza mambo ambayo wanasema na zinaweza kuwasilisha ujumbe kwa Samsung au mashirika yanayohusiana na Samsung kibiashara.
Onyo hilo limetolewa baada ya habari kuchapishwa katika gazeti la mtandao "Daily Beast" iliyochapisha sehemu ya sera za Samsung zinazosimamia umiliki wa kibinafsi wa televisheni zao.
Sera hiyo inaelezea kwamba televisheni hizo zitakuwa zinasikiliza watu katika chumba kimoja wakijaribu kutoa amri na maswali kutumia vibonyezi.
''Iwapo maneno ambayo umeyatamka ni ya kibinafsi au ya kisiri, basi ujue kuwa habari hiyo itakuwa kati ya habari zilizonaswa na kusambazwa kwa watu wengine.'' Samsung imeonya.

Kutokana na kukabiliana kuhusu taarifa ya sera yake, Samsung imetoa taarifa kufafanua jinsi sauti hizo zinavyofanya kazi.
Inasisitiza utambuaji wa sauti unajulikana tu baada ya mmiliki kuchagua kutumia sauti badala ya kubonyeza kifaa cha kiungia mbali (remote control)
Samsung imesema kama mteja atakubali kutumia kifaa cha kugundua sauti, sauti hiyo itatambuliwa na mtu wa upande wa tatu baada ya amri ya kuitafuta sauti hiyo.
Upande watatu ambao unatafsiri sauti kutoka kwa wamiliki hufasiriwa na kampuni inayoitwa Nuance, ambayo imehitimu kutambua sauti.
Samsung si kampuni ya kwanza kujipata mashakani kwa kutumia vinasa sauti kwenye mashine na bidhaa zake.
Mwishoni mwa mwaka wa 2013, mshauri wa maswala ya kiteknolijia kutoka Uingereza aligundua kuwa televisheni yake ya LG ilikuwa inakusanya habari kuhusu tabia yake ya utazamaji wa televisheni.



0 comments:

Post a Comment