Sunday 5 March 2017

MGANGA WA JADI NA ASKOFU AKUTWA NA HATIA YA MAUAJI YA ALBINO AFRIKA KUSINI..

Nchini Afrika Kusini mganga wa jadi ambaye pia ni askofu wa kanisa amepatikana na hatia ya kuwa kinara wa mauaji ya albino, hatua ambayo imepongezwa na Umoja wa Mataifa. 

Ushahidi uliowasilishwa mahakamani ulithibitisha pasipo shaka kuwa kinara huyo Bhekukufa Gumede mkazi wa Kwa-Zulu Natal nchini Afrika Kusini alimwagiza mmoja wa waumini wake alete viungo vya albino ili vitumike kutengeneza dawa za kumpatia utajiri.
Mwezi Agosti mwaka 2015 mwanamke mmoja albino alipotea na ndipo alipatikana baadaye ameuawa na baadhi ya viungo vyake vimechukuliwa.
Akizungumzia uamuzi wa mahakama, mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi, Ikponwosa Ero amepongeza na kusema ni uthibitisho wa uhusiano kati ya mauaji ya albino na ushirikina.
Bi Ero amesema ni hatua bora zaidi kwa kuwa aliyepatikana ni kinara kwani mara nyingi wanaopatikana ni watu wa kati.
Hukumu dhidi ya Gumede inawezakuwa adhabu ya kifo.

0 comments:

Post a Comment