Wednesday 29 March 2017

ABIRIA 141 WANUSURIKA BAADA YA NDEGE KUWAKA MOTO....

Takribani abiria 141 wamenusurika kufa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuwaka moto.

Ndege hiyo ya shirika la Peru, Peruvian Airlines ilishika moto ikiwa angani baada ya kutoka nje ya njia inayotumiwa na ndege kupaa na kutua ambapo Rubani wa ndege hiyo aliielekeza kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Jauja, katika milima ya Andes.

Taarifa zilizotolewa na Shirika hilo la ndege zimesema wazima moto wamefanikiwa kuuzima moto huo na abiria wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo wako salama.

0 comments:

Post a Comment