Matumizi ya bengi kwa kujiburudisha
yatahalalishwa nchini Canada ifikapo tarehe mosi Julai mwaka 2018.
Serikali ya Canada itawasilisha mswada wa kuhalalisha bangi
ifikapo Aprili kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la CBC.
Taarifa ziliiambia CBC kuwa wanachama wa chama tawala cha
Liberal hivi majuzi walijulishwa kuhusu mswada huo.
CBC
imesema kuwa sheria hizo mpya zitaambatana na mapendekezo yaliyotolewa na jopo
lililoteuliwa na serikali.
Baadhi ya mapendekezo hayo ni kuwa Canada itaruhusu kuuzwa kwa
bangi wa kujiburudisha kwa watu walio na zaidi ya umri wa zaidi ya miaka 18,.
Jopo
kazi hilo pia lilipendekeza kuwa watu wazima wataruhusiwa kupanda hadi mimea
minne ya bangi na wamiliki hadi gramu 30 ya bangi iliyokaushwa.
Kwa mujibu wa CBS, serikali itasimamia kusambazwa wa bangi na
kuwapa leseni wazalishaji.
Ahadi
wa waziri mkuu Justin Trudeau, ya kuhalalisha bangi imechochea uvumi katika
sekta hiyo.
Wazalishaji kama makampuni ya Aphria, OrganiGram Holdings, na
Canopy Growth, ambao ni wazalishaji wakubwa zaidi wa bangi ya kutibu, yamekuwa
vipnzi kwa wawekezaji wa hisa.
0 comments:
Post a Comment