Waziri mkuu wa Somalia Hassan ali Khaire, amesema watu mia moja na kumi
wamefariki kutokana na visa vinavyo husiana na ukame na baa la njaa katika eneo
la kusini mashariki mwa nchi hiyo, katika kipindi cha saa nane zilizopita.
Ukame mbaya unaokumba
Somalia unatishia maisha wa mamilioni ya watu nchini humo.
Siku ya Jumanne Rais
Mohamed Abdullahi Farmajo, alitangaza ukame huo kuwa janga la kitaifa.
Umoja wa Mataifa una
kadiria watu milioni tano nchini Somalia, wanahitaji msaada wa dharura na
kuongeza kuwa taifa hilo ni moja kati ya mataifa manne, yaliyo katika hatari ya
kukumbwa na janga la njaa.
Mataifa mengine ni
Nigeria, Sudan kusini na Yemen.
Karibu watu 260,000
walifariki kutokana na baa njaa iliyokumba Somalia kuanzia mwaka 2010 na 2012.
Watu wengine 220,000
walifariki kutokana na njaa ya mwaka 1992.
Pia njaa imetangazwa
katika jimbo la Unity nchini Sudan Kusini, ambayo ndiyo ya kwanza kutangazwa
tangu ile ya Somalia ya mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment