Wednesday 15 March 2017

MAGUNIA 5 YALIYOJAA PESA YAGUNDULIWA UWANJA WA NDEGE

Maafisa wa serikali nchini Nigeria wanasema magunia matano yaliyokuwa na mabunda ya noti, yamegunduliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kaduna.

Pesa hizo zilipatikana katika dawati la kuhudumia wasafiri wanaoingia uwanja wa ndege kuabiri ndege.
Fedha hizo za thamani ya jumla ya dola 150,000 za Marekani, ziligunduliwa wakati wa ukaguzi wa kawaida wa mizigo uwanja wa ndege.
Msemaji wa tume ya uhalifu wa kifedha nchini Nigeria Wilson Uwujaren amesema magunia hayo yalikuwa na mabunda 200 ya noti mpya, ambayo yalikuwa bado hayajafunguliwa kutoka kiwandani.

Amesema uchunguzi unaendelea kubaini nani mwenye magunia hayo.

0 comments:

Post a Comment