Thursday 28 January 2016

SHIRIKA LA NDEGE LAPATA TUZO

Shirika la Ndege la Etihad limetajwa kuwa Shirika la Ndege la
mwaka, kwenye tuzo nyingine za Business Travel 2016.
Tuzo hizo zilitolewa London jana na zilitambua kampuni na watu binafsi, waliopata mafanikio katika sekta ya biashara ya usafiri na hivyo kustahili kuwania tuzo hizo.
Tuzo hizo zinaandaliwa na Jarida la Uingereza la Buying Business Travel, huwa na jopo la wataalamu wanaojadiliana na kisha kupiga kura kubaini washindi.


Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad James Harrison, amesema tuzo hiyo ni ishara ya kutambulika kwa mchango wake katika sekta ya usafiri wa anga.     

0 comments:

Post a Comment