Tuesday 5 January 2016

Mtandao Mtakatifu kuzinduliwa Accra.!

Kundi la RA ambalo ni la Kikristo nchini Ghana, linatarajia kuzindua kmtandao wa kijamii ambao unatajwa kuwa mtakatifu kinyume na uliozoeleka wa Facebook.

Mtandao huo mtakatifu inasemekana utakuwa huru na usioegemea upande wa dini ya Kikristo hata chembe.
Kundi hilo la RA lenye jina LoveRealm, limesema kwamba mitandao ya kijamii imejaa picha zenye maudhui ya utupu na ukatili.
Lakini kundi hilo limejinasibu kuwa mtandao wao ujao, utawasaidia wale ambao walikuwa na mahangaiko ya kulinda imani zao dhidi ya mitandao isiyokuwa na maadili, na mtandao huo utasaidia washirika wake kutubu dhambi miongoni mwao.

Kwa sasa mtandao huo mtakatifu umekwisha waalika maelfu ya wafuatiliaji Wakristo, wafanye majaribio ya kushiriki katika tovuti hiyo katika kituo cha Pentekoste katika mji mkuu Accra.

0 comments:

Post a Comment