Mwanasayansi Dk Derek Lee
amegundua twiga albino kwenye hifadhi ya mbuga ya Tarangire,iliyopo katika Mkoa
wa Arusha nchini Tanzania.
Mtafiti
huyo alipiga picha mbalimbali zikiwa zinamwonyesha mnyama huyo akiwa katika
kundi kubwa la twiga, huku akiwa na rangi ya kipekee ikilinganishwa na twiga
wengine duniani.
Dk
Lee alimgundua twiga huyo wakati akifanya utafiti kwenye mbuga hiyo, na
nyingine za wanyama za barani Afrika.
Taarifa
iliyoripotiwa na shirika la habari nchini Uingereza kupitia gazeti la Dailymail
zimeeleza kuwa, twiga huyo adimu kupatikana duniani iwapo atahifadhiwa atakuwa
kivutio cha pekee katika mbuga hiyo.
Twiga
huyo anayejulikana kitaalamu kwa jina la ‘Omo’ likimaanishwa twiga
mweupe/mwenye ulemavu wa ngozi ‘albino’, alionekana akizunguka katika mbuga hiyo
katikati ya twiga wengine.
Dk Lee ambaye pia ni mtaalamu
wa viumbe na mwanzilishi na mwanasayansi kutoka Wild Nature Instute, alimnasa
twiga huyo katika kamera yake wakati akifanya uchunguzi huo kuhusu wanyama.
AMEsema
uwezekano wa twiga huyo kukua kwa sasa ni mkubwa, lakini bado wanyama wakubwa
wamekuwa wakimwinda na binadamu kwa ajili ya nyama za porini, na huenda rangi
aliyonayo inaweza kumfanya yeye kuwindwa zaidi.
0 comments:
Post a Comment