Wednesday 27 January 2016

TBC KURUSHA MATANGAZO YA BUNGE USIKU...!!


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema kuanzia

mkutano wa 11 wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Television ya taifa  TBC haitaonyesha matangazo ya moja kwa moja kwa muda wote wa vikao.
Waziri Nape amesema hayo leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa ya serikali, na kusema kuwa matukio muhimu ya vikao vya bunge yatakuwa yakirekodiwa na kurushwa katika kipindi maalum usiku katika kituo hicho.
Amesema sababu ya serikali kufanya hivyo ni kupunguza gharama kubwa za uendeshaji, katika kurusha matangazo hayo ya moja kwa moja.
Bonyeza play hapa chini kumsikia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauy akieleza zaidi. 

0 comments:

Post a Comment