Friday 8 January 2016

Perfume inaweza kukuletea balaa..!!

Kama wewe ni kati wale ambao wanakwepa kuoga wakitegemea mtelezo wa Perfume,sikiliza hiii stori tokea huko nchini  Uingereza.


Ni kwamba kijana mmoja Thomas Townsend mwenye umri wa miaka 16, amefariki dunia na uchunguzi unaonesha kuwa, kilichosababisha kifo chake ni matumizi makubwa ya spray za manukato mwilini.

Kijana huyo Thomas alikutwa akiwa amepoteza fahamu chumbani kwake,na baada ya upekuzi wa Polisi walikuta ndani ya chumba chake kuna makopo 42 ya manukato.

Na imeelezwa kuwa ile harufu yenye gesi kwenye manukato hayo,inatajwa kuhusika kusababisha kifo chake.

Mama yake amesimulia pia kwamba mtoto wake hakupenda kuoga, na alikuwa anaweza kupulizia nusu kopo la manukato kwa wakati mmoja..!!

Mtaalam mmoja wa masuala ya afya amesema kijana huyo Thomas,kafariki kutokana na kuvuta hewa ya gesi ya butane inayowekwa kwenye manukato...!!

0 comments:

Post a Comment