Wednesday 20 January 2016

Teknolojia ambazo ni gumzo 2016…

Hexo+
Hiki ni kitu kipya katika nyanja za anga na upigaji picha kufuatia kutangazwa kifaa kinachoitwa Hexo+

Hii ni ndege ndogo isiyo na rubani maarufu kama ‘drone’ iliyofungwa kamera maalumu.
Kinachotokea ni kwamba wewe unapotembea kwenda kokote au unapokuwa kwenye shughuli za burudani, kifaa hiki hii kinakufuata kwa juu au pembeni kwa ajili ya kupiga picha za matukio yote uyafanyayo.
Kifaa hicho ni mapinduzi katika upigaji picha za filamu, huduma za uokoaji, ujenzi na shughuli nyingine zinazohitaji kufuatiliwa na mtu au watu wengi bila kuhitaji mpigapicha kuwa eneo husika. 
Smart Helmet
Kampuni ya vifaa vya kielekroniki ya Marekani Intel, imetengeneza kifaa kinachoitwa Smart Helmet kinachofanya mwaka 2016 uanze vyema.
Kifaa hicho ni aina ya miwani ya macho ambayo inamwezesha mtu kuona ndani ya vitu kama ukuta, mabomba na vinginevyo ambavyo ni muhali kuona ndani.
Kifaa hiki kitasaidia wataalamu wa miamba, wana usalama wanapotaka kuchunguza vitu, wahandisi wa miji na wengine wanaokumbana na changamoto za aina hiyo.
iCar
Tumezoea kusikia na kuona vifaa vya mawasiliano kutoka kampuni ya Apple Inc ya Marekani ikifanya uvumbuzi mkubwa katika vifaa kama simu na kompyuta, lakini sasa mambo yanaanza kubadilika.
Taarifa zinasema kampuni hiyo imeanza majaribio ya gari linalojiendesha lenyewe linaloitwa ‘iCar’, jambo ambalo halikutarajiwa awali. Licha ya mafanikio ya majaribio hayo kutobainishwa, bado kuna picha lukuki zinazoonyesha gari hilo likiwa uwanjani.
Kwa Apple, uvumbuzi huu siyo jambo La kushangaza, kwa sababu walishajikita kwenye teknolojia za mawasiliano, hivyo walichofanya ni kuzihamishia tu katika magari ili kuongeza ufanisi na kuziwahi kampuni nyingine zinazofikiria kuingia katika biashara hiyo.
Ehang 184 flying robot
Ukiachana na Hexo+ kuna ndege nyingine isiyo na rubani iitwayo Ehang 184 flying robot. Hii ni ndege isiyotumia rubani lakini yenye uwezo wa kubeba abiria.
Hii ni ndege ya aina yake iliyotengenezwa na Wachina na uvumbuzi wake umeleta mshtuko katika baadhi ya mataifa yaliyoendelea kiteknolojia.
Habari zinasema unapoingia kwenye ndege hii, unabonyeza programu maalumu yenye taarifa na ramani za maeneo mbalimbali unayochagua kwenda na kisha ndege hiyo inakupeleka bila pasipo shida yoyote.
Hata hivyo, kwa mataifa mengi hofu iliyopo ni ikiwa China itaitumia ndege hiyo kwenye shughuli za kijeshi kwa kusafirisha wanajeshi sehemu mbalimbali za mapambano.
Bimek SLV
Kifaa hiki kazi yake ni kuzuia na kuruhusu au kukata usafirishaji wa mbegu za uzazi. Ni hivi kama kina baba wanataka kuzuia mbegu za uzazi kwenda kwa wanawake wakati wa tendo la ndoa ili kuzuia kizazi, hawatalazimika tena kutumia njia za uzazi wa mpango kama kuvaa kondomu na nyinginezo.
Anachokifanya mwanamume ni kuvaa kifaa hiki, na anapotaka kuzuia mbegu zisipenye atabonyeza kitufe ‘off’ Mgunduzi wa kifaa hiki ni Mjerumani aitwaye Clemens Bimek na kinaweza kuvaliwa na mtu maisha yake yote kama atahitaji kukitumia.
Magurudumu ya kuzalisha umeme
Kampuni ya kutengeneza magurudumu inayoitwa Goodyear imekuja na muundo mpya wa magudumu yanayoweza kuzalisha umeme wakati gari likiwa katika mwendo.


Hii inasaidia iwapo gari litazimika ghafla kwa sababu ya betri au upungufu wa mafuta, basi litawezeshwa kuendelea na safari kwa umbali fulani mpaka der

0 comments:

Post a Comment