Thursday 21 January 2016

Watumiaji wa simu Afrika ni wengi kuliko wanaopata maji salama..!1

Story inayohusiana na maswala ua tafiti leo inagusa Afrika, ikiwa ni ripoti ya utafiti wa Afrobarometer ambayo television ya CNN wameiweka kwenye mtandao wao jana January 19 mwaka 2016.

Ripoti hiyo inaonyesha idadi ya watu ambao wanapata huduma ya majisafi, wenye mawasiliano ya simu za mkononi, umeme na mambao mengine.

Majibu ya ripoti hiyo yanaonesha watu wanaotumia huduma ya simu za mkononi Africa ni 93% ya watu wote waliopo Afrika, wakati huohuo watu wanaopata huduma ya majisafi ni 63%.

Kwenye ripoti hiyo pia inasema kwamba watu wa Afrika 65% wanapata huduma ya umeme, 54% wanatumia barabara zinazopitika, na 30% tu ndio wanaoishi kwenye makazi ambayo yana huduma ya kuhifadhi majitaka (Sewerage)

0 comments:

Post a Comment