Wakati dunia ikiwa na zaidi ya watu 34 milioni wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU), madaktari nchini Hispania wametangaza kugundua tiba ya ugonjwa huo wanayodai ni uhakika.
Kwa kutumia damu ya
kupandikiza kutoka kwenye kitovu mwana (umbilical cord) cha mtu ambaye ana
vinasaba ambavyo havipokei virusi hivyo vya Ukimwi, wataalamu hao wa tiba wa
Hispania wanaamini kuwa wanaweza kutibu ugonjwa huo baada ya mafanikio
waliyopata kwa mgonjwa mmoja.
Madaktari hao wa
Kitengo cha Taifa cha Upandikizaji (ONT) cha Hispania, walichukua damu ya
vitovu mwana vya watu wenye vinasaba ambavyo havipokei VVU na kuipandikiza kwa
mtu anayeishi na virusi hivyo.
Baada ya miezi
mitatu mgonjwa huyo alipimwa na kuonekana hana virusi.
Daktari wa Programu
ya Upandikizaji kutoka Taasisi ya Tiba ya Catalan Barcelona Rafael Duarte, amesema
mgonjwa aliyetibiwa kwa njia hiyo Timothy Brown (37), alikuwa anaishi na VVU
tangu mwaka 2009, na madaktari hao walithibitisha kuwa amepona baada ya
kupandikizwa damu hiyo.
Mgonjwa mwingine
aliyefanyiwa majaribio ya tiba hiyo alipona VVU, lakini miaka mitatu baadaye
alifariki kwa ugonjwa wa saratani.
Timu ya madaktari wa
Hispania ililiambia gazeti la kila siku nchini humo la El Mundo kuwa wana
uhakika kuwa wameleta mapinduzi katika mapambano ya Ukimwi na magonjwa
yanayofanana na hayo.
Dk Duarte amesema
mwaka 2015 umekuwa wa kujivunia ugunduzi huo mkubwa duniani, ingawa
alitahadharisha kuwa tiba kamili haiwezi kupatikana katika siku za usoni.
0 comments:
Post a Comment