Tuesday 26 January 2016

WASICHANA BIKIRA KUSOMESHWA BURE.!!

Mashirika ya kutetea haki za binaadamu nchini Afrika Kusini, yanasema yamekasirishwa na mpango wa

kuwapa ufadhili wa elimu ya vyuo vikuu wasichana 16 ikiwa watabakia bikira.

Wasichana kutoka wilaya ya Uthukela ya mkoa wa mashariki wa KwaZulu-Natal, wana fursa ya kupewa msaada wa elimu wa hadi miaka mitatu, ili kugharamia masomo yao katika chuo kikuu.
Meya wa eneo hilo Jabulani Mkhonza amesema kuwa, wasichana wanaishi katika hatari kubwa ya kunyanyaswa, kupata mimba na hata kuambukizwa virusi hatari vya Ukimwi.

Lakini wapinzani wanasema mpango huo ni wa kuwadunisha wanawake, wakiongeza kuwa pesa za walipakodi hazipaswi kutumiwa kukiuka haki za wasichana.

0 comments:

Post a Comment