Thursday 28 January 2016

KENYA YASHIKA NAFASI YA 139 KWA UFISADI...

Shirika la Transparency International, juzi lilisema kuwa kiwango cha ufisadi kimekuwa kikiongezeka katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Taarifa hiyo ilisema kwamba Rwanda na Tanzania ndiyo mataifa yameibuka kuwa bora katika utekelezaji wa mambo kwa njia ya uwazi, katika kanda ya nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Transparency International, nchi ya Kenya inashika nafasi ya 139 kwa ufisadi ulimwenguni.
Aidha shirika hilo lilitoa pendekezo la Serikali ya Kenya, kuweka mikakati ya kushirikisha na asasi nyingine kando na EACC kukabiliana na ufisadi nchini humo.
Shirika hilo liliongeza kusema kwamba ipo haja kwa Idara ya Sheria, kuharakisha mchakato wa kusikilizwa kwa kesi zinazohusu ufisadi nchini humo.
Mkurugenzi Mkuu wa Transparency International Kenya Samuel Kimeu, amesema mchango wa idara hiyo ni muhimu ikiwa ufanisi kamili utapatikana katika vita hivyo.
Shirika hilo lilisema ikiwa nchi hiyo itaamua kuwakamata na kuwafikisha mahakamani kisha sheria zikachukuliwa, basi hata maendeleo ya nchi yataonekana.
Taarifa hiyo ilisema baada ya kukamilisha utafiti huo kwa ujumla, nchi ya Kenya ilipata wastani wa asilimia 25 sawa na ilivyokuwa mnamo 2014.     

0 comments:

Post a Comment