Thursday 7 January 2016

Mtoto apewa jina la timu ya mpira bila mama yake kujua..!!

Shabiki mmoja wa Arsenal alifanikiwa kumshawishi mkewe wampe mtoto wao jina la Arsenal bila mwanamke huyo kugundua hilo.

Ilikuwa ni baada ya miaka miwili ambapo mwanamke huyo Clare Smith, alijulishwa ujanja ambao mumewe alikuwa ametumia.
Bi Smith kutoka eneo la Black town jimno la New South Wales nchini Australia, alifichua hayo kwenye barua aliyoandikia jarida moja, ambapo amesema mwenyewe hakugundua hilo hadi mumewe alipomwambia.
Amesema waliamua kumwita binti yao Lanesra, kwa sababu lilikuwa jina la kipekee na la kupendeza.


Lakini bint yao alipotimiza umri wa miaka miwili, ndipo mume wangu akanifichulia kwamba lilikuwa jina la Arsenal ukiandika kutoka nyuma.

0 comments:

Post a Comment