This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Wednesday 27 February 2013

Hivi ni vivutio vya Tanzania vilivyoingia katika maajabu saba ya asili Afrika. Serengeti Migration, Mlima Kilimanjaro na Ngorongoro crater.

Ni Katika kile kinyang'anyiro cha kupata vivutio asilia saba vyenye maajabu toka barani Afrika. Kinyang'anyiro ambacho kilirindima mwaka jana 2012 kwa wadau kupigia kura vivutio 11 vilivyokuwa vikishindanishwa. Mlima Kilimanjaro,Wanyama wanaohama wa Serengeti na Ngorongoro crater ndio yalikuwa maajabu toka Tanzania ambayo yalikuwa yameteuliwa kupigiwa kura,kwa kifupi vivutio vyote vitatu toka Tanzania vimeweza kufanya vyema. Taarifa ya vivutio vitatu kutoka Tanzania kuingia kwenye orodha ya vivutio 7 vya ajabu barani Afrika iliwekwa wazi mjini Arusha,ambako kulikuwa na sherehe rasmi ya kuvitaja vivutio vilivyoingia kwenye orodha hii baada ya zoezi la kupiga kura kusitishwa mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka 2012. Katika hafla hiyo,Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndio alikuwa mgeni rasmi. Matokeo hayo yalitangazwa na Dk,Phillip Imler ambaye ni rais wa taasisi ya Seven Natural wonders of the world. Vivutio vingine viliweza kuingia kwenye orodha hii ni Okavango Delta, Red Sea Reef, Jangwa la Sahara na Mto Nile. Tanzania ndio nchi pekee iliyoweza kuingiza vivutio 3 kwenye orodha hii kwa mwaka 2012. Kiwale11 Bloga inatoa pongezi kwa wote waliotikia wito na kupiga kura na kuiwezesha nchi yetu kutoka kifua mbele kwa kuingiza vivutio 3 kwenye orodha hii.

Mazoezi makali yanaongezea umri?..

Wewe ni mkimbiaji au muinua vyuma? Wakimbia katika mbio za masafa marefu au katika mashindano ya michezo mitatu tofauti - triathlon? Ni mazoezi yapi ambayo unaweza kufanya ikiwa unataka kujiongezea umri? Je, ni vyema zaidi kufanya mazoezi mafupi na makali, au marefu zaidi lakini ya taratibu? Kwa mujibu wa Daktari Jamie Timmons, Profesa wa masomo ya bayologia ya uzee katika Chuo Kikuu cha Birmingham, dakika tatu za mazoezi makali kila juma kwa majuma manne kunaweza kukaboresha, kwa kiwango kikubwa, afya ya mtu. Mazoezi haya makali yanaweza kusaidia moyo na mapafu yako kusambaza hewa mwilini vyema zaidi. Pia yanaboresha ifanyavyokazi insulini, ambayo inaondoa sukari mwilini na kudhibiti mafuta. Nao utafiti wa Daktari Stuart Gray wa Chuo Kikuu cha Aberdeen unadhihirisha kwamba mazoezi makali na mafupi, kama kukimbia kwa kasi kwa masafa mafupi, au kuendesha baiskeli kwa sekunde 30 tu, kunaufanya mwili uondoe mafuta kutoka kwenye damu haraka zaidi kuliko kufanya mazoezi ya wastani, kama kutembea harakaharaka. Kuondolewa kwa mafuta kutoka kwenye damu ni muhimu kwa vile kunapunguza uwezekano wa kukumbwa na tukio la mshtuko wa moyo.

WABUNGE WAZICHAPA WAKATI WA MDAHALO KWENYE TV.SHOW

a href="http://3.bp.blogspot.com/-hxnIUxxpXgM/US4zIp1YMoI/AAAAAAAAAPM/oHNMGfzY9MY/s1600/wabunge.jpg" imageanchor="1" > Wabunge wawili wapigana makonde wakati wa kipindi cha mdahalo kwene runinga ya kitaifa huku Georgia. Huko Lebanon wabunge wengine wawili pia warushiana glasi za maji na baadae kupigana ngumi vilevile wakati wa mdahalo kwenye Televisheni. Hii ni baada ya wabunge hao kuhitalafiana kuhusu vita vinavyoendelea nchini Syria baina ya waasi na serikali ya Rais Basher al Assad.