Wednesday 7 March 2018

UNAFAHAMU UMRI SAHIHI WA KUANZA KUFANYA MAPENZI NCHINI MWAKO..?

Ufaransa inatarajia kuweka sheria maalum ya umri wa kuanza kufanya mapenzi kuwa ni miaka 15.

Hivyo kufuatia mapendekezo hayo mtu yeyote atakayebainika kufanya mapenzi chini ya umri huo atakuwa amebaka.

Maamuzi haya yamekuja nchini humo mara baada ya madaktari na wanasheria kutoa ushauri wao kuhusiana na umri mtu anaostahili kuanza kufanya mapenzi.

Hata hivyo wakati msimamo huo ukitolewa huko nchini Ufaransa, hali ni tofauti katika maeneo mengine barani Ulaya.
Ulaya:
Austria,Ujerumani,Italia ni miaka 14,Ugiriki, Poland, Sweden ni miaka 15,Ubeligiji, Netherland, Spain, Urusi na Uingereza ni miaka 16.
Barani Afrika:
Miaka 12 Angola, Miaka 13 Burkina Faso, Comoro, Niger, Miaka 14 Botswana (wanaume), Cape Verde, Chad (wasichana), Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (wasichana), Lesotho (wanaume), Madagascar na Malawi,Miaka 15 Guinea, Morocco, Miaka 16 Algeria, Botswana (wanawake), Cameroon, Ghana, Guinea Bissau, Lesotho (wanawake), Mauritania, Mauritius, Mozambique, Namibia, Senegal, Afrika kusini, Swaziland, Togo, Zambia, Zimbabwe.
Miaka 18 Benin, Burundi, Afrika ya kati,Ivory Coast, DRC (wanaume), Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gabon, Gambia, Kenya, Liberia, Mali, Nigeria, Republic of Congo, Rwanda, Seychelles, Sierra Leone, Somalia, South Sudan, Tanzania, Uganda, Miaka 20 Tunisia.Katika vigezo hivyo vya umri, Angola ikiwa ni nchi pekee ya barani Afrika iliyoweka umri mdogo zaidi ya watu kujihusisha na ngono wa miaka 12.Na kwa upande wa Umoja wa mataifa hakuna sheria au muongozo maalum kuhusu umri ambao unaruhusu mtu kuanza kufanya tendo hilo, licha ywa kwamba kuna haki za kumlinda mtoto.

0 comments:

Post a Comment