
Tanzania, Burundi na Rwanda zimeorodheshwa
kuwa kati ya nchi zenye watu wasio na furaha duniani katika orodha ya kila
mwaka ya Umoja wa Mataifa kuhusu viwango vya furaha duniani.Burundi ndilo
taifa ambalo wakazi wake hawana furaha zaidi duniani katika nafasi ya 156
ambapo imechukua nafasi hiyo kutoka kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR)
iliyokuwa inashikilia nafasi hiyo mwaka jana.CAR ndiyo
inayoifuata Burundi katika orodha ya mwaka huu.Tanzania
imeshika nafasi ya 153 sawa na mwaka jana huku Rwanda pia ikishikilia nafasi ya
151 sawa na mwaka jana kati ya mataifa 156.Orodha ya mwaka
jana hata hivyo ilishirikisha mataifa 155.Taifa
linaloongoza kwa furaha duniani mwaka huu ni Finland, kwa mujibu wa ripoti hiyo
ya UN ambapo nchi hiyo imechukua nafasi hiyo kutoka kwa Norway.Ripoti hiyo
huangazia furaha waliyo nayo watu wa taifa furahi na chanzo cha furaha hiyo.Mataifa ya Ulaya
Kaskazini yanashikilia nafasi tano za juu kwa kuwa na viwango vya juu vya raia
walioridhika, huku nchi zilizoathiriwa na vita vya muda mrefu pamoja na nchi
kadha za Afrika Kusini mwa Sahara zikiendelea kwa mara nyingine kushikilia nafasi
tano za chini.
0 comments:
Post a Comment