Chama tawala nchini Burundi CNDD/FDD kimemtangaza
Rais Pierre Nkurunzinza, kama kiongozi mkuu wa kudumu au kiongozi wa milele
ndani ya chama hicho.
Uamzi huo umefikiwa baada ya vikao vya siku tatu vya
mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika katika eneo la Buye anakozaliwa Bwana
Nkurunziza Kaskazini mwa nchi hiyo.
Uamuzi huo pia unachukuliwa wakati Burundi
inajiandaa kufanya marekebisho ya katiba, ili kumruhusu Rais Nkurunzinza kuendelelea
kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.
Taaarifa ya chama cha CNDD/FDD imesema kuwa, vikao
hivyo vilinuwia kuimarisha chama tawala na taasisi zake.
0 comments:
Post a Comment