Monday 5 March 2018

INSPEKTA WA POLISI NA WAZIRI WA ULINZI WAFUKUZWA KAZI…

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amemfuta kazi Inspekta mkuu wa polisi Kale Kayihura na waziri wa Ulinzi Henry Tumukunde.

Generali Kayihura ambaye ni mkereketwa wa vita vilivyomsaidia rais Museveni kuingia madarakani mwaka 1986, kwa wakati mmoja alikisiwa kuwa afisa mwenye mamlaka makubwa zaidi katika jeshi la Uganda.
Lakini amekabiliwa na shinikizo kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu wa usalama.
Zaidi ya wanawake 20 wameuawa katika visa vya mauaji, ambavyo havijatatuliwa katika maeneo yanayouzunguka mji mkuu wa Kampala, na katika miezi mitatu iliyopita raia watatu wa kigeni pia wameuawa.
Naibu wake Okoth Ochola anashikilia wadhifa huo.
Kwa mujibu wa ujumbe alioandika rais Museveni katika mtandao wa Twitter, amesema: "Kwa uwezo wa mamlaka niliyopewa kikatiba, nimemteua Jenerali Elly Tumwiine kama waziri wa usalama.Nimemteua pia bwana Okoth Ochola kama afisa mkuu wa polisi. Niabu wake atakuwa ni Brigedia Sabiiti Muzeei.
Mnamo Mei mwaka 2017 Rais Museveni alimteua upya Kayihura kama mkuu wa polisi kwa muhula mwingine wa miaka mitatu hadi mwaka 2020.

Uteuzi huo ulikumbwa na mzozo na haukudumu.

0 comments:

Post a Comment