Tuesday 6 March 2018

VIDEO: MOTO WATEKETEZA SOKO LA MBAGALA….

Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu–Dar, asubuhi ya leo Machi 6, 2018.


Sehemu iliyoathirika zaidi ni ya wauza mitumba huku baadhi ya bidhaa zao zikiteketea kwa moto lakini hakuna aliyeripotiwa kupoteza maisha wala kujeruhiwa.

Chanzo cha moto huo kinadhaniwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo tayari gari la jeshi la zima moto limefika  kuzima moto huo.

0 comments:

Post a Comment