Wabunge
wa kambi ya upinzani katika Bunge la Kosovo wamefyatua gesi ya machozi bungeni
wakati vikao vya bunge vikiendelea, kwa lengo la kuzuia bunge hilo kupitisha
mkataba wasioupenda.
Wapinzani
walifanya tukio hilo kama njia ya kuvuruga zoezi la upigaji kura kupitisha
mkataba wa ujirani kuhusu mpaka kati ya nchi hiyo na Montenegro.
Kipande
cha video kilichoonekana kwenye mitandao ya kijamii kinawaonesha wabunge
wakitoka ndani ya bunge hilo wakiwa wanajifuta macho na kufunika pua zao
kutokana na madhara ya gesi hiyo.
Kwa
mujibu wa naibu spika wa bunge hilo, Avni Bytyci gesi hiyo ilifyatuliwa na
mbunge wa upinzani, Levizja Vetvendosje.
“Mkataba
wa mpaka kati yeu na Montenegro utapitishwa na bunge leo licha ya wabunge
wachache wa upinzani kutaka kuvuruga kikao kwa kutumia njia ya vurugu,” alisema
Bytyci.
Mkataba
huo utawapa nafasi wananchi wa Kosovo kupata Visa bure ya kusafiri katika nchi
za umoja wa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment