Tuesday, 6 March 2018

WACHUNGAJI 6 WA MAKANISA YALIYOFUNGWA RWANDA WAKAMATWA..

Polisi nchini Rwanda imetangaza kuwatia kizuizini wachungaji 6 na viongozi wa makanisa, kutoka baadhi ya makanisa yaliyofungwa kwa amri ya serikali ya nchi hiyo.

Wiki iliyopita serikali ya nchi hiyo iliamrisha kufungwa kwa makanisa zaidi ya 700, kwa madai ya kutotimiza kanuni za ujenzi wa makanisa yao.
Miongoni mwa waliokamatwa ni kasisi Askofu Innocent Rugagi, kiongozi wa kanisa la Abacunguwe ambaye ni mojawapo ya wachungaji mashuhuri nchini Rwanda.
Polisi inawashutumu kwa kufanya mikutano ya siri kukaidi uamuzi wa serikali.

Askofu Rugagi alisikika akishutumu kile alichokitaja kuwa uamuzi wa ghafla kuyafunga makanisa bila ya ilani ya kutosha.Jumla ya makanisa 700 yamefungwa, mengi yakiwa ni makanisa madogo madogo yaliyoanzishwa hivi karibuni.Reactions:

0 comments:

Post a Comment