Sunday 4 March 2018

MWANAMUME AJIPIGA RISASI NA KUJIUA NJE YA WHITE HOUSE….

Mwanamume mmoja amejipiga risasi na kujiua nje ya Ikulu ya Marekani ya White House mjini Washington, kikosi cha kumlinda rais kimesema.

Kikosi hicho kilisema kuwa mwanamume huyo alikaribia ua unaozunguka Ikulu katika barabara ya Pennsylvania kabla ya kuchomoa bunduki na kupiga risasi mara kadhaa.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa, kulingana na polisi.
Rais Donald Trump hakuwa kwenye Ikulu. Yuko katika kasri lake la Mar-a-Lago huko Florida.
Mwanamume huyo alikuwa kwenye watu wengi wakati alipiga risasi, kulingana na wale walioshuhudia,na jina lake bado halijatangazwa.
Video iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter ilionyesha watu wengi wakikimbia kutoka eneo hilo.
Kumekuwa na visa kadha vinavyohusu usalama katika Ikulu ya White House miaka ya hivi karibuni.

Cha hivi karibuni tarehe 23 Februari, gari liliendeshwa kwenda kwa kizuizi cha Ikulu ambapo mwanamke wa miaka 35 alikamatwa.

0 comments:

Post a Comment