Monday 11 May 2015

Korea Kaskazini yazindua Silaha kali…

Serikali ya Korea Kusini inasema inaamini kuwa Korea Kaskazini,inaweza kumiliki nyambizi kadha za kufanya mashambulizi kutoka baharini ndani ya miaka mitano ijayo.

Hii ni baada ya Korea Kaskazini kuchapisha picha zilizomuonyesha kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un akitazama majaribio ya kuizindua nyambizi hiyo.
Korea Kusini imezikagua picha hizo za uzinduzi kwenye vyombo vya habari vya Korea Kaskazini na kusema kuwa ni za kweli.
Korea Kusini imesema kuwa uzinduzi huo ni suala linalochukuliwa kwa umakini na tahadhari kubwa sana.
Sasa Korea Kusini na Marekani zinafikiria kuweka ngao ya mitambo ya kuzuia makombora kutoka Kaskazini hatua itakayogharimu mabilioni ya pesa.
Hata hivyo haijulikani ikiwa makombora yanayofyatuliwa na nyambizi hiyo yana uwezo wa kubeba silaha za nuklia.
Wadadisi wanasema kuwa Korea Kuskazini inaonekana kufanya mambo kwa kasi zaidi,kuliko ilivyokisiwa kuunda zana zilizo na uwezo wa kushambulia kwa haraka.

0 comments:

Post a Comment