Wednesday, 20 May 2015

Obama ajiunga na Twitter..!!

Rais wa Marekani Barack Obama amejiunga na mtandao wa twitter, ikulu ya White House imethibitisha
Rais wa Marekani Barack Obama amejiunga na mtandao wa twitter, ikulu ya White House imethibitisha.
Akitumia anuani @POTUS (President Of The United States) Obama tayari amewavutia wafuasi 1.7 milioni moja nukta saba.

"Hamjambo, Twitter!Ni Barack.
Kwa hakika baada ya miaka 6 hatimaye wameniruhusu kujiunga na mtandao wa Twitter''Obama alisema kwenye ujumbe wake wa kwanza.
Obama alikuwa na anuani tofauti inayomilikiwa na wahudumu wa ikulu yake .Anuani hiyo inawafuasi Milioni 59.3m.
Anuani hiyo @BarackObama ilizinduliwa mwaka wa 2007, na kila akituma ujumbe anaanza na BO.
" Anuani ya @POTUS itamruhusu Obama kuwasiliana moja kwa moja na mamilioni ya wafuasi wake'' ilisema taarifa ya White House
Obama hakuweza kuwa na simu ya mkononi kutokana na itifaki na usalama
"Rais Obama angependa serikali yake iwe ya wazi @POTUS na hii ndio jukwaa mwafaka ya mazungumzo."
Kwa sasa rais Obama amewafuata watu 65 wakiwemo rais wa zamani wa Marekani ,Bill Clinton, George Bush na mkewe mwenye anuani ya kipekee @FLOTUS.
Hata hivyo hajamfuata Hillary Clinton wala waziri mkuu wa Uingereza David Cameron.
Tayari mawasiliano yake na Bill Clinton yamezua mjadala Clinton akimtania kwa kumuuliza iwapo ataondoka na anuani hiyo atakapo achia ngazi.

Related Posts:

  • Je wajua siri ya Mamba usingizini….? Wataalamu wa masuala ya wanyama wamegundua kwamba, mamba ana uwezo wa kulala huku jicho lake moja likiwa wazi. Utafiti huo ambao umewaacha wengi wakishangaa, kwani picha nyingi duniani huonyesha kuwa mamba hulala fofofo,… Read More
  • Je Aspirin inazuia kurejea kwa Saratani…..? Utafiti mkubwa na wa kwanza kubaini iwapo umezaji wa tembe za Aspirin kila siku unapunguza kwa kiwango kikubwa athari ya kurejea kwa saratani umeanza nchini Uingereza. Jaribio hilo litahusisha watu 11,000 wanaotibiwa a… Read More
  • Usikose nakala yako ya gazeti la TABIBU kesho alhamisi likiwa limesheheni habari kemkem za afya. Ni kwa bei ya sh. 500/= tu. TABIBU michezo wiki hii.!! … Read More
  • Bibi wa miaka 85 akamatwa kwa kuiba herein…….. Bibi kizee mmoja mwenye umri wa miaka 85 raia wa Marekani, na ambaye amekuwa akiiba vito vya thamani kwa zaidi ya miaka 60 amehukumiwa tena kwa kosa la wizi. Doris Payne anatuhumiwa kwa wizi wa herini ya thamani ya dol… Read More
  • Filamu mpya ya Stars Wars yavunja rekodi… Filamu mpya ya Star Wars: The Force Awakens imevunja rekodi Uingereza kwa kuuza tikezi nyingi zaidi siku ya kwanza ya kuuzwa kwa tiketi. Tiketi hizo za mapema zilianza kuuzwa Jumanne, huku filamu hiyo ikitarajiwa kuto… Read More

0 comments:

Post a Comment