Wednesday 20 May 2015

Nkurunziza ahairisha uchaguzi…!!





Rais wa Burundia Pierre Nkurunziza amehairisha uchaguzi wa ubunge kwa siku kumi.
Msemaji wa rais Willy Nyamitwe ameiambia shirika la habari la AFP
kuwa,kufuatia jaribio la mapinduzi juma lililopita na vurugu zilizofuatia ni bora kuahirisha uchaguzi huo kwa muda.
''Uchaguzi huo wa ubunge ulikuwa umeratibiwa kufanyika tarehe 26 mwezi Mei,lakini sasa inatubidi kuihairisha ili kuwasikiza washirika wetu wa kimataifa pamoja na tume ya uchaguzi ambayo pia inatumia muda huo kutatua maswali yaliyoulizwa na vyama vya upinzani.'' alisema Nyamitwe.
Hadi kufikia sasa tarehe rasmi ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanywa Juni tarehe 26 haijabadilika.
Umoja wa mataifa ya bara Ulaya EU na Umoja wa mataifa ya Afrika AU, yametoa wito kwa uchaguzi huo uliokumbwa na utata mkubwa uhairishwe ilikutoa fursa kwa mazungumzo ya upatanishi kuendelea.
Takriban watu laki moja wamekimbilia mataifa jirani wakihofia kutibuka upya kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

0 comments:

Post a Comment