Bilionea muasisi wa Tesla Elon Musk, anasema kuwa betri hiyo mpya itawezesha watu wengi kupata afueni kutokana na kuwa na uhakika wa nguvu za umeme bila ya kukatizwa.
Anasema kuwa teknolojia hiyo mpya itabadilisha mtizamo wa watu Duniani wa namna ya kutumia umeme.
Tesla inapanga kwanza kuuza betri hizo nchini Marekani, mnamo miezi michache ijayo.
Tesla tayari inatengeneza betri zinazotumiwa na magari ya umeme yasotumia petrol.
Betri hizo aina ya lithium-ion huchajiwa mara-kwa-mara.
Kwa teknolijia hio betri za kutumia majumbani na katika biashara zinatengenezwa
Mfumo huu wa betri unaitwa Powerwall wa vizio aina mbili: kizio cha 7kWh chauzwa $3,000 ilhali kizio cha 10kWh kwa $3,500.
Inakisiwa Tesla itachuma $4.5bn kwa mauzo hayo.
Lakini wadadisi wanadhani huenda Tesla ukakumbwa na ushindani mkubwa na makampuni mengine yenye masilahi hayo, kama General Elecctric na LG ya Korea Kusini.
0 comments:
Post a Comment