Wednesday, 20 May 2015

Watinga kuchukua maiti wakivalia nguo za magunia……….

Ilikuwa ni kama kutekeleza maandiko ya Biblia yanayosema “jifungeni nguo za magunia, ombolezeni na kulia kwa uchungu”, wakati ndugu walipokwenda Hospitali ya Rufaa ya KCMC kuchukua mwili wa marehemu.

Walikuwa wamevalia magunia, lakini sababu ya kuvalia nguo hizo haikuwa kama maandiko hayo yanavyosema kuwa “kwa sababu hiyo jifungeni nguo za magunia; ombolezeni na kulia kwa uchungu; kwa maana hasira kali ya Bwana haikugeuka na kutuacha”.
“Tumejiuliza maswali mengi, tumeshindwa kupata majibu. Tumejiuliza tuvae nguo gani hatukupata majibu.
Kwa kuvaa hivi tunataka hao wauaji wajue damu hii itawalilia popote walipo,” alisema Beata Kiria, ambaye ni dada wa Victoria Sylvester aliyeuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kuzikwa nusu kiwiliwili.
Beata na ndugu zake walifika kwenye hospitali hiyo kwa ajili ya kuuchukua mwili huo wakiwa wamevalia magunia.
Tukio hilo lilitokea jana kati ya saa 4:30 asubuhi na saa 6:00 mchana wakati ndugu hao walipofika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali, huku baadhi yao wakiwa pekupeku na kusababisha watu wengi waliokuwa eneo hilo pamoja na watumishi wa hospitali kuwashangaa.
Wakiwa ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti, ndugu hao walilia wakipaza sauti wakitaka wauaji wa mwanamke huyo wakamatwe kabla ya kuchukua mwili na kuondoka nao.
Victoria (53), mkazi wa Kijiji cha Masherini Umbwe eneo la Kibosho,aliuawa kwa kukatwa mapanga usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita na baadaye wauaji kuuzika mwili wake nusu na kuacha kiwiliwili nje ya nyumba waliyokuwa wakiishi, jambo lililoibua utata mkubwa ndani ya familia hiyo.
Kiria amesema walichagua mavazi hayo baada ya kukosa vazi lingine.
Imezoeleka misiba mingi ndugu huvaa suti nyeusi kwa wanaume huku wanawake wakivalia mavazi meusi au meupe ambayo baadaye hujifunika na vitambaa vyeusi au vyeupe kwa akina mama.
Kiria ambaye alizungumza kwa niaba ya familia, alilitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha linawatafuta na kuwakamata watu waliohusika na mauaji hayo.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani,amesema wanamshikilia mume wa marehemu Silvester Mmasi na mtumishi wao ambaye hakumtaja kwa ajili ya mahojiano kuhusu mauaji hayo na polisi inaendelea kuwatafuta washukiwa wengine.

Related Posts:

  • TIMU ZILIZOINGIA ROBO FAINALI EURO 2016.... Michuano ya Euro 2016 hatua ya 16 bora ya imemalizika tayari na hizi ndo timu ambazo zimesha ingia robo fainali baaada ya June 27 2016 kuchezwa michezo miwili ya mwisho. Mechi za robo fainali zitaanza kuchezwa June … Read More
  • ITALIA YAWATAKA WATENGENEZA PIZZA KUSOMA ZAIDI….. Kundi la maseneta wa Italia wametoa wito kwa watengenezaji wa Pizza nchini humo, kupasi mitihani yao ili kuboresha viwango vya uandaaji wa mlo huo. Wabunge 22 katika bunge la juu wamewasilisha mswada bungeni ambao ukipi… Read More
  • UKIJAAMIANA NA UNDER 18 JELA INAKUITA..…! June 27 2016 bunge la 11 limefanya mapitio ya marekebisho ya muswada wa sheria ya mtoto, ambayo imeelekeza kuwa mtu atakayempa mimba mtoto ambaye kisheria anafahamika ni yule mwenye umri wa chini ya miaka 18, basi atahu… Read More
  • ALIMWA KADI NYEKUNDU KWA KUPUMUA MBELE YA MWAMUZI….! Mchezaji wa Sweden ameonyeshwa kadi nyekundu baada ya mwamuzi kumtuhumu kuwa alifanya vitendo visivyokuwa vya ‘kiungwana’ na ‘kiuanamichezo’ uwanjani. Adam Lindin Ljungkvist anayeichezea Pershagens SK, alikuwa uwanjani k… Read More
  • WAZIRI MKUU WA UINGEREZA AJIUZULU….! Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika muungano wa Ulaya. Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini kw… Read More

0 comments:

Post a Comment