Tuesday 19 May 2015

Wanawake Rombo wakodi wanaume Kenya.....!!!





Mkuu wa Wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo, amesema tatizo la ulevi kupindukia Wilayani humo limewaathiri wanaume kiafya na kuwataka watendaji kulivalia njuga.

Kutokana na ulevi huo kuna madai kwamba baadhi ya wanawake wanaoishi kwenye ndoa, wamelazimika kutafuta wanaume nchi jirani ya Kenya ili wapate mimba kutokana na wanaume zao kuzidiwa na ulevi hivyo kushindwa kuwahudumia.
Kipuyo amesema tatizo la ulevi limefikia hatua ya hatari zaidi na jitihada za haraka zinahitajika.
Kipuyo ametaja maeneo yaliyokithiri kwa ulevi ni kilelewa ambapo ni mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Amesema ni vizuri mamlaka husika na Serikali ya vijiji kuhakikisha ulevi unakwisha ili kuepuka Wilaya hiyo kuwa na kizazi cha Wakenya.

0 comments:

Post a Comment