Utakumbuka vizuri kuhusiana na lile tukio lililotokea kule Nchini Uganda, la cha msichana wa kazi kumtesa mtoto wa bosi wake kwa kumpiga.
Hilo likiwa bado halijasahaulika tukio la aina hiyo limetokea tena kule nchini Bulgaria, baada ya muuguzi Emiliya Kovacheva kumtesa kwa kumpiga mtoto mchanga wa siku nne bila kuwa na huruma kwa madai anapiga kelele.
Mtoto huyo Nicole aliyekuwa ameachwa na mama yake, alipata majeraha makubwa kufuatia mateso kutoka kwa muuguzi huyo.
Awali muuguzi huyo alikataa kuwa amefanya kosa hilo, lakini baadaye alikiri baada ya kuonyeshwa video baada ya kamera kunasa tukio zima ndani ya chumba hicho cha hospitali.
Muunguzi huyo alisema alifanya hivyo kutokana na kuchanganyikiwa baada ya mtoto huyo kukataa kulala na kuwasumbua watoto wengine waliokuwa wamelala.
Kutokana na kitendo hicho, muugzi huyo kwa sasa anakabiliwa na kosa la mauaji.
0 comments:
Post a Comment