Thursday 14 May 2015

Breaking: Burundi watu wote ndani, Wanajeshi kwa Wanajeshi wanapambana.

Kutoka Bujumbura Burundi taarifa za sasa ni kwamba raia wameamriwa kutotoka nje, milio ya risasi inasikika, Wanajeshi watiifu wa Rais wanapambana na waliompindua.

Makundi hasimu ya askari yanakabiliana katikati mwa mji mkuu wa Burundi- Bunjumbura, mahala ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais Pierre Nkurunziza, amepinduliwa.
Makabiliano ya risasi yanaendelea kwa sasa, huku milipuko kadhaa ikisikika.
Radio na runinga ya taifa inang'ang'aniwa kwa sasa huku wanajeshi waaminifu kwa rais Nkurunziza ndio wanaoidhibiti.
Kingine ni kwamba kituo binafsi cha Radio kilichotumika kutangaza mapinduzi ya Kijeshi kimechomwa moto saa tisa usiku wa kuamkia leo na Wanajeshi wanaomtii Rais.



0 comments:

Post a Comment