Wednesday 13 May 2015

Mkenya kunyongwa China…………..!



Mwanadada mwenye umri wa miaka 26 huenda akanyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa ya kulevya nchini china ambapo Mkenya huyu Floviance Owino,
aliyehudumu kama msaidizi wa nyumbani alitiwa nguvuni May 2013 akisafiri kuelekea Beijing kutokea hapa Nairobi.
Afisi ya ubalozi wa kenya nchini Uchina umethibitisha kwamba, huenda Floviance akanyongwa mwaka huu baada ya kifungo chake cha miaka miwili kukamilika na haya maneno ni kwa mujibu wa dada yake ambaye ni Judith Owino.
Judith anasema hakufahamu kuwa dada yake alikuwa amesafiri kwenda China hadi alipopata habari kutoka kutoka ubalozi wa kenya nchini humo.
Serikali ya uchina hata hivyo ilimwarifu Judith kwamba alikuwa na muda mfupi kugeuza hukumu hiyo na kuzuia dada yake asinyongwe, walimshauri atafute wakili hivyo kwa sasa anahitaji visa kwenda china maana mda unazidi kupotea.
Mpaka sasa Judith hajapata fursa ya kuzungumza na Floviance kwani serikali ya china haikukubali hilo lifanyike.

0 comments:

Post a Comment